Tuesday, May 2, 2017

DKT NCHIMBI: MWAJIRI NA MWAJIRIWA SI MTU NA ADUI YAKE
Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi afisa wa usalama kutoka shirika
la TANESCO Mkoa wa Singida Juma Mauba zawadi ya cheti na TV flat
screen baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora mwaka 2017.
Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa ameshikama na Mwenyekiti wa
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Singida Aaran Jumbe (kulia
kwake) na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (kushoto kwake) wakiimba wimbo
maalumu wa wafanyakazi wa Mshikamano daima pamoja na wimbo wa taifa.
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi kwa Mkoa wa Singida.
Watumishi
wa Kutoka Halmashauri ya Ikungi wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi na kuonyeshwa mazao ambayo huzalishwa kwa wingi wilayani humo
ambayo ni viazi vitamu na alizeti katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa
Mkoa kwa Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akitoa
zawadi ya mpira kwa viongozi wa wafanyakazi wanawake kwa halmashauri zote saba
za Mkoa wa Singida ili waweze kuunda timu za wanawake katika halmashauri zao.
Waajiri wote Mkoani Singida hususani wakurugenzi wa
halmashauri ambao ndio wenye watumishi wengi wameelekezwa kujenga mahusiano
mazuri baina yao ili kuboresha utumishi wao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa
maelekezo hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani hapa
yaliyofanyika katika uwanja wa Peolpe’s mjini Singida.
Dkt. Nchimbi amesema mwajiri na mtumishi sio maadui
bali wanapaswa kujenga mahusiani mazuri hasa kwa mwajiri kujenga mazoea ya
kufahamu sifa za watumishi wake, shida na matatizo yao.
Ameongeza kuwa waajiri wamekuwa wakisubiria
watumishi wakosee ndio wawape adhabu lakini haipaswi kuwa hivyo kwani mwajiri
anatakiwa ahakikishe anaweka mazingira mazuri na kumuelimisha mtumishi asifanye
makosa.
“Ukiona mtumishi anafanya mambo yanayokinzana na
sheria, kanuni na utaratibu, usimkaripie wala kumtega, mtafutie afisa ustawi wa
jamii. Kwa vyo vyote afisa ustawi wa jamii atamrejesha kwenye mstari stahiki na
mambo yatakwenda vizuri”.
Aidha Dkt Nchimbi amewataka wakurugenzi kutofanya
ziara nyingi nje ya halmashauri zao bali wajikite katika kusikiliza na kutatua
kero za wananchi na watumishi wao ambazo watazibaini endapo watafanya ziara za
kutosha katika halmashauri zao.
Amesema ili kuboresha maslahi ya watumishi, waajiri
wanapaswa kuandaa mafunzo kwa watumishi juu ya matumizi bora ya fedha ili
waweze kutunza fedha zao, kila halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya
watumishi kupewa viwanja vya makazi pamoja na kila halmashauri kuwa na afisa
ustawi wa jamii atayehusika na watumishi kwa ajila ya masuala ya ushauri.
Pia Dkt. Nchimbi amekemea tabia mbaya ya baadhi ya
wakuu wa idara/vitengo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wafanyakazi wa
kike walio chini yao.
“Wakuu hawa wa idara/vitengo wanakiuka sheria
kanuni na taratibu kwa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi humo humo kazini.
Wakati mwingine wanafanya mapenzi na wake za watu. Tabia hii haikubaliki na
haivumiliki hata kidogo. Viongozi au wakuu wa idara/vitengo wenye tabia ya aina
hii, waiache mara moja”, amesema Dk.Nchimbi.
Kwa upande wao wananchi na watumishi Mkoani Singida
wamempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kwa hatua zake utumishi wa umma ambapo kwa sasa amerejesha nidhamu na uadilifu
kwa kiwango cha kuridhisha.
Wananchi hao wamesema chini ya serikali ya awamu ya
tano watumishi wa umma wamebadilika sana na sasa wanatoa huduma kwa ukarimu
mkubwa, wepesi na uharaka zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
“Huko nyuma watumishi wa umma wengi walikuwa wana
urasimu wa hali ya juu. Walikuwa wakitoa huduma huku macho na akili zao zikiwa
kwenye ‘whatsapp’. Mbaya zaidi mwananchi ukipeleka kero zako, wanakuona ni
msumbufu. Hivi sasa mambo ni tofauti kero za wananchi zinatafutiwa majibu na
majawabu kwa wakati,” ameongeza Dkt. Nchimbi akiunga mkono maoni ya wananchi.
Mmoja wa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo
Sombi Hangida amekiri kwamba ni kweli watumishi wa umma wamebadilika mno na
sasa wanatoa huduma bila kuomba rushwa na wamekuwa na lugha rafiki kwa
wananchi.
Awali mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya
wafanyakazi TUCTA Mkoani Singida Aaran Jumbe amehimiza kuhusu mabaraza ya
wafanyakazi kufanyika katika maeneo ya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na
taratibu na hasa kuwashirikisha vyama vya wafanyakazi.
Jumbe ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikitoa
ushirikiano kwa vyama vya wafanyakazi na kuomba ushirikiano huo uendelee huku
akisisitiza zawadi za mfanyakazi hodari zinazo ahidiwa na taasisi na
halmashauri zitolewe kwa wakati.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 2, 2017
Older Article
Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Yaanza Mwanza
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment