Exim Bank Tanzania yatoa fursa ya ziara kwa wanafunzi wa Harvard - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, May 15, 2017

demo-image

Exim Bank Tanzania yatoa fursa ya ziara kwa wanafunzi wa Harvard


1

Benki ya Exim Tanzania hivi karibuni imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa wanafunzi waliokuwa wanafanya ziara ya kimasomo kutoka chuo kikuu maarufu cha biashara cha Marekani – Harvard Business School. Wanafunzi hao walikuja katika benki hiyo jijini Dar es Salaam kwa wiki moja kama sehemu ya mafunzo yao ya mwaka wa kwanza kupitia mpango unaoitwa ‘FIELD Global Immersion’ ambayo Exim ni mmoja wa wanachama.

“Tunajivunia kufanya kazi pamoja na chuo cha Biashara cha Harvard kwa kuwapatia wanafunzi uzoefu wa kihalisia wa kufanya kazi katika nchi kama Tanzania” alisema Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Fredrick Kanga. “Tuna uhakika kupitia ziara hii wanafunzi hawa waliweza kupata ujuzi ambao wasingeweza kupata katika majadiliano ya darasani pekee.”

Mpango huo wa FIELD Global Immersion ni programu iliyoundwa kuwaimarisha wanafunzi na kuwajengea uwezo wao wa kumudu na kuweza kufanya kazi kiufanisi katika tamaduni mbalimbali ulimwenguni.

Photo-2

Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu maarufu cha biashara cha Marekani – Harvard wakizungumza na wananchi.

Benki ya Exim ilianza kufanya kazi na wanafunzi hao kwa miezi kadhaa kabla ya kuwasili nchini. Wakiwa nchini wanafunzi hao walitoa mawazo yao kwa uongozi, walishiriki katika utafiti na wateja jijini Dar es Salaam na mwishowe kutoa mapendekezo yao kwa uongozi wa benki. Kusudio la zoezi hili ni kutoa fursa kwa wanafunzi kupata uzoefu wa kufanya kazi katika mradi wa uvumbuzi katika mazingira mageni.


Harvard inakiri pia kuwa ziara hii ya kimasomo isingewezekana bila kuwepo na washirika wa kimataifa. “Tunaishukuru sana Exim Bank Tanzania na washirika wengine wote wa FIELD Global Partner kwa yale wanayofanya kwa niaba ya wanafunzi wetu,” alisema Profesa Juan Alcacer, mkuu wa kitengo cha FIELD. “Wanafunzi wetu wanafaidika kupita kiasi kupitia ziara hizi na tunategemea kuwa washirika wetu wanafaidika pia.”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *