Mmoja wa viongozi wa vijana wa Chama cha Tanzania
Girl Guides (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa (kulia), akilakiwa na Katibu wa Taifa
wa TGGA, Grace Shaba baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana.
KIONGOZI wa Vijana wa
Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa
amefanya kazi kubwa ya kuwashawishi Wananchi wa Mexico kuwa Mlima Kilimanjaro
upo Tanzania badala Kenya.
Dk. Mutasingwa ambaye
alikuwa nchini Mexico kwa mafunzo ya miezi minne ya kubadilishana uzoefu katika
nyanja za utamaduni na uongozi alitumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya
Tanzania.
Akizungumza mara
baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,
alisema kuwa moja ya mambo yaliyompa wakati mgumu ni kuwabadilisha wamexico
kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya kama wanavyofahamu wao.
Alisema Wamexico wengi kwanza wanajua Afrika ni nchi, jambo ambalo pia ilibidi awaeleze kuwa siyo nchi bali ni bara kama yalivyo mabara mengine duniani na katika bara hilo kuna nchi nyingi na mojawapo ni Tanzania anayotokea yeye.
Alisema Wamexico wengi kwanza wanajua Afrika ni nchi, jambo ambalo pia ilibidi awaeleze kuwa siyo nchi bali ni bara kama yalivyo mabara mengine duniani na katika bara hilo kuna nchi nyingi na mojawapo ni Tanzania anayotokea yeye.
Alisema akiwa huko licha
ya kuwafundisha kiswahili pia alitangaza vivutio vingi vya utalii
vilivyopo nchini, ambapo aliwatajia wadudu, ndege za kila aina na wanyama
mbalimbali waliomo kwenye hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na
nyinginezo.
Pia aliwafundisha kuhusu utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili, upikaji wa vyakula vya kitanzania kama vile ndizi na pilau, mambo ambayo walifurahishwa nayo.
Pia aliwafundisha kuhusu utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili, upikaji wa vyakula vya kitanzania kama vile ndizi na pilau, mambo ambayo walifurahishwa nayo.
Dk. Mutasingwa alisema
kuwa ambaye katika ziara hiyo ya mafunzo alikuwa na vijana wenzie wa Girl Guids
kutoka Venezuela, Canada, Uingereza na Argentina alipata wasaa wa
kujifunza utamaduni wa mexico na kutoka nchi hizo zingine.
Alisema kuwa alijifunza
mambo mengi ikiwemo ujasiri wa kufanya kazi bila woga, siasa za mataifa
mbalimbali, mambo ambayo ameahidi kuwafundisha vijana wenzie wa TGGA hapa
nchini.
Dk. Mutasingwa aliwasili nchini jana, ambapo kwenye Uwanja wa Ndege wa JNIA,
alilakiwa na Katibu wa Kitaifa wa TGGA, Grace Shaba pamoja na wanachama wenzie
Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi.
Dk. Mutasingwa akiwa na Katibu wa TTA Taifa, Grace Shaba (kushoto), Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi baada ya kulakiwa
akitokea Mexico
Dk Mutasingwa akikumbatiana kwa furaha na Maryrehema
Kijazi
Dk. Mutasingwa akifurahia jambo na Elieshupendo
Michael na Maryrehema Kijazi.
Ni
furaha iliyoje kukutana
Dk. Mutasingwa akifurahi wakati akilakiwa na
Elieshupendo Michael
Grace Shaba na Dk. Mutasingwa wakiwa na furaha
No comments:
Post a Comment