Mchimbaji mdogo wa Madini ya Almas ambaye pia ni Mshauri Mwelekezi wa
SANA Gems Gregory Kibusi, akiangalia ubora wa Madini ya Alamsi.
Mshauri Mwelekezi wa SANA
Gems Gregory Kibusi, (kulia), akionesha madini ya Almas. Katikati ni Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza Kishan Bhatti.
Madini ya Almas ambayo bado hayajasanifiwa.
Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini ya Almas (TANSORT) kutoka Wizara ya
Nishati na Madini Archard Kalugendo (kulia) akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo (kushoto) namna ya kupima ubora wa Madini ya Tanzanite.
Mjiolojia kutoka Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Jumanne Shimba,
akiangalia madini kwa kutumia kifaa maalum cha kinachotumiwa na kituo hicho
katika mafunzo.
Mnunuzi wa Madini ya Tanzanite (kushoto) akiangalia ubora wa Madini ya
Tanzanite katika Banda la Kampuni ya TanzaniteOne. Kulia ni Mwakilishi wa
Kampuni ya TanzaniteOne.
Watumishi kutoka Kituo
Cha Jemolojia Tanzania (TGC), wakimsikiliza mgeni aliyembelea banda la kituo
hicho ili kujua shughuli za mafunzo ya usanifu na unga’rishaji wa madini
zinavyofanyika. Mikufu inayoonekana katika picha pamoja na mapambo mengine
imetengenezwa kituo hapo. Kituo hicho kiko chini ya Wizara ya Nishati na
Madini.
Ujenzi wa kisima cha maji kilichojengwa na Kampuni ya SANA Gems Ltd
ikiwa ni sehemu ya kuwezesha jamii inayozunguka mgodi wa kampuni hiyo kunufaika
na uwepo wa mgodi husika.
Wachimbaji wadogo wa
Madini walioshiriki Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito, Arusha
wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji bora na uhifadhi wa mazingira
kwa wachimbaji nchini.
Ombi hilo lilitolewa na Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya SANA Gems, ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini ya Almas, Gregory Kibusi.
Kampuni ya SANA Gems
inayofanya shughuli zake za uchimbaji mkoani Shinyanga ndiyo kampuni pekee ya
wachimbaji wadogo iliyokuwa ikionesha madini ya Almas katika Maonesho hayo.
Kibusi aliongeza kuwa,
ushiriki wa wachimbaji katika maonesho hayo ni fursa kwao ya kukutana na
wanunuzi na kujenga mtandao wa kibiashara hivyo kuiomba serikali kuendelea
kuwahamisha wachimbaji wadogo nchini kushiriki katika maonesho hayo kwa kuwa,
yanawezesha uhakika wa masoko ya madini yao.“Nikiwa pia kama Katibu Mkuu wa
wachimbaji wadogo Shinyanga, natoa wito kwa wachimbaji nchini kutumia vyama
vyao washiriki maonesho haya ya Arusha kwa kuleta madini yao. Soko la uhakika
lipo,” alisema Kibusi.
Aidha, Kibusi alitumia
fursa hiyo kuwataka wachimbaji nchini kuachana na matumizi ya zebaki na
kuwataka kutumia njia bora zinazoelekezwa na Serikali. Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh, alisema kuwa, kampuni hiyo imeshiriki
Maonesho hayo ili kuweza kujenga mtandao wa kibiashara ikiwemo pia kutoa fursa
kwa Watanzania kujifunza namna Madini ya Almas yanavyochimbwa na mahali
yanapopatikana.
Aidha, ameitaka Serikali
ifikishe umeme katika eneo hilo na maeneo mengine mbapo shughuli za uchimbaji
mdogo zipofanyika ili kuwezesha kuharakisha maendeleo ikiwemo kuwezesha
shughuli za kiuchumi na kupanua wigo wa ajira.
Akizungumzia namna
kampuni hiyo inavyosaidia eneo linalozunguka mgodi wake alisema kuwa, kampuni
hiyo imetengeneza kisima cha maji kwa ajili ya kijiji cha Hukiro pamoja na
kuboresha baadhi ya miundombinu katika zahanati iliyo jirani na mgodi wa
kampuni hiyo
Maonesho ya 6 ya
Kimataifa ya Vito Arusha yalifunguliwa rasmi tarehe 3 Mei na Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Dkt. Joel Bendera na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
No comments:
Post a Comment