Kamati ya Miss Tanzania
kwa kushirikiana na kampuni ya Grace Product na Gift Jewelers wamekabidhi gari
kwa Mrembo wa Shindano hilo Diana Edward Lukumai ambaye alishinda taji la
Miss Tanzania 2016/2017.
Akizungumza wakati wa
kukabidhiwa zawadi hiyo Miss Diana amesema kuwa anaishukuru sana kamati
hiyo kwa kumsaidia kupata zawadi hiyo ambayo ameisubiri kwa hamu na kwa muda
mrefu .
“Wasichana wanatakiwa
kuwa wavumilivu na kujiandaa kisaikolojia kwani kushinda taji la urembo la Miss
Tanzania sio kitu kidogo, watu wengi watakufuatilia, hivyo lazima ujitambue
kuwa ukiwa Miss Tanzania ni mtu ambaye anatakiwa kuwa msiri, hivyo
wasichana wajiandae sana kisaikolojia katika hili.” Amesema Miss Diana.
Amesema kuwa gari hiyo
itaweza kumsaidia katika matumizi yake binafsi hasa katika kipindi hiki ambacho
anaendelea na kampeni yake ya Dondosha wembe ambayo ina lengo la kumkomboa mtoto
wa kike juu ya mila potofu za kuozeshwa mapema na ukeketaji.
Kwa upande wake mkuu wa
itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albart Makoye amesema mara baada ya
kukabidhi kwa zawadi hiyo kunafungua pazia la shindano jipya la mwaka 2017/2018
.
Amesema kuwa warembo
wanatakiwa kujiweka sawa hili waweze kunyakuwa taji hilo ambalo mashindano yake
yataanza kuanzia ngazi ya votongoji mpaka taifa.
Ofisa wa
Basata akikabidhi funguo kwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai kama
ishara ya kumkabidhi mrembo huyo gari yake aina ya Suzuki Swift pembeni
yake Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili.
Miss
Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akiingia ndani ya gari yake mara baada ya
kukabidhiwa.
Miss
Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akifurahi mara baada ya kuingia ndani ya gari
yake.
Mkuu wa
Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania , Arbart Makoye akizungumza na Waandishi wa
habari mara baada ya kukabidhi gari.
Mkurugenzi
wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili na Mumewe wakikabidhi kadi ya gari
kwa Miss Tanzania 2016/217 Diana Lukumai.
Mkurugenzi
wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili. akizungumza na Miss Tanzania 2016/2017
Diana Lukumai katika duka la ke lililopo City Mall jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment