Mratibu Abdulfareed Hussein akiwa
katika picha ya pamoja na waimbaji wa bendi za DDC Mlimani Park
"Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma"
wakijiandaa na mpambano wa kumsaka Mkali nani Mei 20 mwaka huu.
Mratibu Abdulfareed Hussein
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mpambano wa kumsaka mkali wa
muziki wa dansi baina ya DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae"
na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Pembeni
ni viongozi na waimbaji wa bendi hizo kulia ni Abdallah Hemba kutoka
Sikinde na kulia ni Meneja wa Bendi ya Msondo Said Kibiriti.
Muimbaji wa bendi ya Sikinde
Abdallah Hemba akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina
yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Kushoto ni Mratibu Abdulfareed
Hussein.
Meneja wa Bendi ya Msondo Said
Kibiriti akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina
yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu akiwa sambamba na waimbaji wa timu
hiyo Romario na Juma Katundu.
HISTORIA inaendelea tena
kuandikwa baada ya bendi kongwe mbili za muziki wa Dansi nchini DDC Mlimani
Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma"
zitakutanishwa tena katika jukwaa moja kumtafuta nani mkali wa kulisakata rumba
Mei 20 mwaka huu.
Bendi hizo kongwe
zitakutana tena katika jukwaa moja na kumtafuta nani mkali huku kila
upande ukitamba kumgaragaza mwenzake na kuibuka kidedea katika mpambano huo.
Pambano hilo linatarajiwa
kufanyika Mei 20 Mwaka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni huku mashabiki
wa kila upande wakiombwa kuja kuhudhuria kwa wingi kuwaona wakali hao huku
burudani za nyimbo za zamani zikiratajiwa kutawala kwenye usiku huo.
Akizungumza kuelekea
pambano hilo, mratibu Abdulfareed Hussein alisema mpambano huo wa nani zaidi
utamuliwa na mashabiki wa dansi watakaojitokeza siku hiyo na zaidi kutakuw ana
zawadi ambayo ni siri itakayotolewa siku hiyo.
Alisema kiingilio cha
pambano hilo kitakuwa ni Sh. 10,000 ili kuwapa nafasi wadau wa dansi kushuhudia
na kutoa maamuzi ya nani zaidi kati ya bendi hizo mbili.
"Hili pambano ndio
litakata mzizi wa fitna, ambapo mashabiki ndio wataamua nani zaidi kati ya
Msondo au Sikinde kwani ni muda mrefu sana hawajakutana jukwaa moja "
alisema.
Wakati huo huo Mmoja
wakilishi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema wamejiandaa vizuri kutoa burudani
na kuhakikisha kwamba wako vizuri kuliko Msondo.
"Hawa jamaa
wametukimbia sana, hivyo kila tunapotaka kukutana nao wanakuwa na safari naona
Mei 20 ndio mwisho wao," alisema.
Nao Meneja wa Msondo,
Said Kibiriti alisema wamejiandaa vyema hivyo katika pambano hilo wataimba
nyimbo mchanganyiko na zaidi kambi hyao itakuwa Pemba na wanawaahidi mashabiki
wa bendi yao kuja kwa wingi.
"Tutaimba nyimbo
mchanganyiko, pia tutaimba nyimbo zetu mpya, tunaamini mpambano huo ndio
utaweza kuamua nani kati yao ni zaidi," alisema Kibiriti.
No comments:
Post a Comment