Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC,
Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na
Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.
MWALIMU Commercial Bank
PLC imezindua kampeni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi
kwa ujumla.
Akizungumza kwenye
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati
akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw.
Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na
watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au
anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.
Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja anapoweka akiba
(fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja
itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema, kadiri Mteja
anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi
mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000
na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4) na kujishindia
zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki
hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu
na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa
serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua
Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.

Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo,
Bw. Valence Luteganya, akifafanua jinsi kampeni hiyo itakavyofanyika.
Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma
Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo.
Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi.
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
No comments:
Post a Comment