Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala
Group Gavin Halliday
Shirika la Anga la Etihad
(EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Hala Group ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji wake na kuimarisha huduma
zake ulimwenguni.
Halliday ataliongoza
shirika hilo katika kuendana na huduma bora ulimwenguni ikiwa ni pamoja na
kuwasogeza karibu wateja na kuendelea kufurahia huduma bora zinazotolewa na
shirika hili pamoja na washirika wake wa ndege. Pia, atawajibika kuwa karibu na
wabia wa EAG pamoja na kushiriki vikao vya utawala ambavyo ni ndiyo nguzo
muhimu kwa mipango na maendeleo ukuaji wa biashara ya usafirishaji Abu Dhab na Nchi
za Falme za Kiarabu.
Halliday anaungana na
Shirika la Anga la Etihad baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa
akifanya kazi kwa miaka 30 katika Shirika la Ndege la Etihad na kwenye Shirika
la IAG. Kwa miaka mitatu ya hivi karibuni amekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Avios,
ambayo ni programu maarufu ulimwenguni. Pia amewahi kuwa katika nafasi ya juu
akihusika na masuala ya biashara kwenye Shirika la IAG, Iberia, British Midland
na British Airways.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Anga la Etihad, H.E Mohomed Mubarak Fadhel Al Mazrouei alisema,
“Hala ni nembo muhimu kwa Etihad ambayo imekuwa ikihakikisha inawaunganisha
wabia wetu kwenye biashara ya usafiri wa anga. Pia ni idara muhimu ambayo
imekuwa kiungo muhimu kwa wasafiri wa Abu Dhab na Nchi za Famlme za Kiarabu
kwenye biashara na usafirishaji wa uhakika. Gavinni ni miongoni mwa watu muhimu
kwenye sekta hii ya usafiri wa anga, hivyo tunafurahia kujiunga na timu ya
uongozi wa EAG.
“Tumefurahishwa na uzoefu
wa Gavin na tunaamini ataendeleza programu za masoko ulimwenguni jambo ambalo
ndiyo mpango wetu mkubwa.”
Halliday alisema, “Hii ni
nafasi ya heshima niliyoteuliwa. Shirika la Ndege la Etihad ni miongoni mwa
makampuni yanayokuwa kwa kasi kwenye sekta ya anga katika karne hii. Hala ndiyo
kitovu cha ukuaji huo. Ninatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na mashirika ya
ndani ya usafirishaji na kupanua biashara na kuwavutia wasafiri wengi Abu Dhabi
na Nchi za Falme za Kiarabu.”
Hala ilianzishwa mwaka 2016 ili kutekeleza mipango ya EAG ya kutoa huduma bora zaidi katika, usafirishaji na kibiashara. Hii inajumuisha Global Loyalty, Etihad Holidays, Hala Abu Dhabi, Hala Traveli Management na Amadeus Joint Venture.
Hala ilianzishwa mwaka 2016 ili kutekeleza mipango ya EAG ya kutoa huduma bora zaidi katika, usafirishaji na kibiashara. Hii inajumuisha Global Loyalty, Etihad Holidays, Hala Abu Dhabi, Hala Traveli Management na Amadeus Joint Venture.
Halliday ataanza rasmi
majukumu yake mwezi Septemba mwaka huu.
Mabadiliko hayo, Halliday
anachukua nafasi ya Darren Peisley ambaye kwa sasa ana kaimu nafasi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Hala.
HE. Al Mazrouei
alimshukuru Peisley kwa machango wake alioutoa akisema kwamba, “Darren amefanya
mambo mengi mazuri akiwa Hala. Amekuwa mwanzilishi na kuimarisha biashara ya
Global Loyality na kuitambulisha ulimwenguni ambapo hadi sasa inahudumia zaidi
ya wananchama zaidi ya milioni 20.
Pia awali alipokuwa
akiongoza idara ya biashara na aliwezesha kufanya mabadiliko kwa kipindi cha
miaka saba akiwa na Shirika la Ndege la Etihad. Tunamshukuru kwa mchango wake
na tunamtakia kila heri katika utendaji wake hapo baadaye atakaporudi
Austaria.”
No comments:
Post a Comment