Monday, May 15, 2017

TANESCO yatoa tahadhari juu ya mvua zinazoendelea
SHIRIKA la Umeme
Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa
taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua au
sababu nyingine.
Akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, alisema,
sambamba na hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu
ya umeme.
“Lakini tunawaomba
wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko wa maji
mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.
Dkt. Mwinuka pia alisema
endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na
kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa ili kuwapa hadhari
wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa TANESCO
wakichukua hatua za marekebisho.
Mamlaka ya Hali ya Hewa
nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa
maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa
na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50.
Aidha kwa upande wake,
mtaalamu wa masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo,
amewahakikishia wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na
hitilafu zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za
kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na magari, au
miti kuangukia nguzo.
"Naomba nitoe
angalizo kwa wateja wetu, kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani
kwako, ni vema ukatoa taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye
taaluma badala ya kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna
utaalamu na masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."
Naye kaimu Meneja
Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika kipindi hiki cha mvua kuna
athari ndogo ndogo zimetokea kwenye miundombinu ya TANESCO hususan nguzo za
umeme, lakini akatoa hakikisho kuwa mafundi wa TANESCO wanekuwa wakichukua
hatua za haraka kurekebisha athari katika miundombinu ya umeme pindi tu
zinapotokea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Dkt. Mwinuka ametoa tahadhari kwa
wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au
kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha
mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na
kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu
kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea
Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji,
akitoaufafanuzi zaidi wa hatua za kuchukua endapo wateja au wananchi wataona
hitlafu ya umeme kwenye maeneo yanayowazunguka
Mhandisi Kihiyo, (kulia) na Kaimu Meneja Uhusianowa
TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari
Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu Meneja Uhusiano wa
TANESCO, Leila Muhaji (kushoto) na Afisa Uhsiano wa Shirika hilo, Henry
Kilasila wakijadiliana jambo.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
KILUPI: ATAKA KURA ZA MAONI ZISIWAGAWE WANACCM
Hassani MakeroApr 14, 2025Dkt.Dimwa - Akemea Rushwa Mchakato wa Kura za Maoni
Hassani MakeroApr 14, 2025WAZIRI ULEGA AWAOMBA TET KUENDELEZA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU
Hassani MakeroApr 14, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment