May
12, 2017 Chelsea
imecheza mchezo wa Ligi Kuu England
dhidi ya West Brom
ambapo bao pekee la Michy Batshuayi limeiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa
wa Premier League msimu
wa 2016/2017 katika mchezo uliopigwa The Hawthorns.
Batshuayi alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika nane mchezo
kumalizika katika mchezo ambao Chelsea ilihitaji
ushindi ili kutwaa ubingwa wa EPL
ikifikisha point 87 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikibakiwa na
michezo miwili kumaliza ligi.
Kwa
kutwaa ushindi huo, Chelsea
chini Antonio Conte
imeweka rekodi ya kuwa klabu ya pili kutwaa ubingwa wa EPL mara nyingi ambapo imetwaa
mata tano nyuma ya Manchester United iliyotwaa mara 13.
Chelsea imeweka pia rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutwaa
ubingwa wa EPL
siku ya Ijumaa tangu Arsenal
ilipofanya hivyo katika uwanja wa Anfield
1989 huku Antonio Conte akiwa meneja wa nne kutoka Italia kushinda taji hilo baada
ya Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.


No comments:
Post a Comment