Wananchi wa waishio Lushoto wamepatwa na adha ya usafiri baada ya mvua zinazoendelea kusababisha kuporomoka kwa mawe na udongo na kufunga maeneo yenye njia za mawasiliano
Wor'Out Media Blog ikiongea na mmoja wa wananchi waishio maeneo hayo ya Vuga, Ndugu Raphael Rahim Mgongo, anasema mvua hizo zimepelekea kudhorotesha uchumi wa sehemu hiyo.
Wasafiri wakipita katika barabara iliyomegwa na maporomoko ya mvua eneo la Vuga Bazo Lushoto Mkoani Tanga na kuhatarisha usalama kwa watembea kwa miguu.
Wanafunzi na wasafiri wanaoelekea Lushoto wakipanda moja ya mawe yaliyofunga barabara baada ya kuanguka juu mlimani kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juzi.
No comments:
Post a Comment