Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili
Msanii maarufu nchini wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili
umekamilika.
Wakili wa
Serikali, Onolina Moshi aliyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mheshimiwa,
kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika naomba
ahirisho kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH). Amesema
Moshi.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Juni Mosi, 2017 kwa PH.
Wema
amewakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.
Mbali na Wema
washtakiwa wengine ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida
Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima.Watuhumiwa hao wawili
wanatetewa na wakili Peter Kibatala na Hekima Mwesigwa.
Wema ambaye
ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 alifikishwa
mahakamani hapo na kupandishwa kizimbani baada ya kusota mahabusu katika kituo
kikuu cha Polisi (Police Central) Dar es Salaam kwa muda wa siku Sita.
Awali
ilidaiwa kuwa, Februari 4 mwaka huu, huko Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni,
washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili.
Hata hivyo
washtakiwa hao wote walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana.

No comments:
Post a Comment