Wanaotumia bahari wametakiwa kuchukua tahadhari
Tanzania
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi,
Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka hiyo, kupitia taarifa, imesema kunatarjiwa kuwepo na
upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2.
"Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa
mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania," mamlaka
hiyo ilisema.
"Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo yaliyotajwa
wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki."
Hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei.
No comments:
Post a Comment