Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia)
akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB
Business Club' waliokutanishwa na benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha
Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano
wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club' waliokutanishwa na NMB jana
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili
kukuza biashara zao.
Baadhi ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo
na ukuaji wa biashara zao.
Sehemu ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo.
Baadhi ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za
mikopo na ukuaji wa biashara zao.
Sehemu ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akizungumza kufungua mkutano wa
wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na
benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara
pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha
Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano
wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club' waliokutanishwa na NMB jana
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili
kukuza biashara zao.
Afisa
Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela akizungumza
na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa "NMB
Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani
wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa NMB Business Club Mkoa wa Dar es Salaam, Ezekiel Gutti akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa '"NMB
Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani
wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara
jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo.
BENKI ya NMB imekutanisha
wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya
wafanyabiashara wa NMB "NMB Business Club" kwa lengo la kutoa mafunzo
mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao.
Kundi hilo la NMB Business Club
mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa pamoja ili wafanyabiashara hao waweze
kujuana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao jambo ambalo litachangia
wao kushikamana na kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Akizungumza na wafanyabiashara
katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati,
Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo wataalam wa biashara wa Benki ya
NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna ya kukuza biashara na kuelezea fursa
anuai zilizopo ndani ya benki hiyo ili wateja wao waendelee kunufaika nazo.
Alisema mbali ya kutoa mafunzo ya biashara na kodi wana NMB Business Club
walioshiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya
huduma wanazopewa ili benki iangalie namna ya kuzishughulikia.
Awali
mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana
akifungua mkutano huo aliwataka wafanyabiashara hao kutambua kuwa Serikali
inawategemea wafanyabiashara katika kukuza jiji kupitia huduma mbalimbali za
kibiashara ambzo wanazitoa kwa jamii.
Alisema
Serikali kupitia ofisi yake itaendelea kujenga mazingira bora ya
wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa maendeleo na kuwaomba walipe kodi
kama inavyotakiwa kwenye biashara zao, kwani hii ndio njia pekee ya kuboresha huduma
na maendeleo kwa jamii.
"...Mtambue
ya kwamba katika huduma mnazozitoa kibiashara mbali ya kunufaika nyinyi
mnachangia kuleta maendeleo, pia mnapendezesha jiji letu...inapaswa mtambue ni
watu muhimu sana katika kujenga uchumi," alisema Mkurugenzi huyo wa jiji
la Dar es Salaam. Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa NMB Business Club Mkoa wa
Dar es Salaam, Ezekiel Gutti alisema wafanyabiashara walioalikwa katika mkutano
huo ni ambao wamekuwa wakinufaika na huduma mbalimbali za mikopo na ushauri wa
kifedha kutoka kwa benki ya NMB na wanafanya vizuri katika biashara zao na hata
marejesho kwa mikopo mbalimbali wanayoomba benki.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akizungumza kufungua mkutano wa
wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na
benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara
pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
No comments:
Post a Comment