Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka
17 'Serengeti Boys
TIMU
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeendeleza wimbi
la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu katika mechi za kimataifa katika
maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 yatakayoanza
mwezi Mei 14, 2017 baada ya jana kuwafunga wenyeji, Cameroon 1-0 mjini Yaounde.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ahmadou Ahijo, mjini Yaounde na kuhudhuriwa na
gwiji wa soka wa Cameroon, Rogger Milla, bao la Serengeti Boys limefungwa na
Ally Ng'anzi dakika ya 36.
Serengeti
Boys ilitua Younde, Cameroon Alhamisi ikitokea mjini Rabat, Morocco ambako
iliweka kambi ya karibu mwezi mmoja na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Gabon na kushinda 2-1 kila mchezo.
Kwa
ujumla Serengeti Boys imekwishacheza mechi tano tangu kuanza kambi rasmi ya
maandalizi fainali za Gabon, baada ya awali kuifunga Burundi mara mbili, Machi
30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa
Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’
Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada
ya mchezo wa leo, Serengeti Boys inatarajiwa kurudiana na Cameroon Mei 3, mwaka
huu kabla ya Mei 7 kwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za
Mali, Niger na Angola.
Cameroon
nayo itashiriki fainali hizo ikiwa imepangwa Kundi A lina timu za wenyeji,
Gabon, Guinea na Ghana.
No comments:
Post a Comment