Rais Donald Trump na Rais Xi jinping
Rais wa Marekani, Donald Trump
amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuiunga mkono Marekani na jitihada zake
za kupambana na mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini.
Trump amesema kupata
ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza
Beijing kuhusu masuala ya biashara.
Rais Donald Trump amesema
aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka,
mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un.
''Rais wa China, Rais Xi,
ninaamini amekuwa akimshinikiza pia.lakini mpaka sasa, pengine hakuna
kilichotokea na pengine kimetokea. Hili lilikua kombora dogo, halikuwa kombora
kubwa, halikuwa jaribio la Nuklia, ambalo alitegemewa kulitekeleza siku tatu
zilizopita, tutaona nini kitakachoendelea''.
Trump ametahadharisha kuwa
mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni
ya watu.
Aliyasema hayo kwenye mahojiano
na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya mvutano
iliopo kati ya nchi yake na Korea kaskazini.
Rais Kim Jong Un
Trump amesema rais wa Korea kkaskazini,
Kim Jong Un ameendelea kubaki kwenye utawala wa Korea kaskazini, ingawa
wamekuwepo wale ambao wangeweza kumpinga ''alikuwa kijana mdogo wa miaka 26 au
27 hivi, alipochukua mamlaka kutoka kwa baba yake, baba yake alipofariki.
Ni wazi kuwa anakabiliana na
watu wenye nguvu zao, majenerali na wengine. Katika umri huo mdogo, aliweza
kuchukua madaraka. Watu wengi, nina uhakika, walijaribu kuyachukua madaraka
hayo, pengine, mjomba wake au mtu mwingine yeyote. Hivyo ni wazi kuwa ni kijana
mwerevu, lakini tuko kwenye hali ambayo hatuwezi kuifumbia macho, hatuwezi
kuruhusu kilichokuwa kikiendelea kwa miaka mingi kiendelee''.
Siku ya jumapili,Kiongozi huyo
wa Marekani alizungumza na Mawaziri wakuu wa Thailand na Singapore kujadili
namna ya kuishinikiza Serikali ya rais wa Korea kaskazini, Kim Jong.
No comments:
Post a Comment