SHIRIKA la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha Afya
katika Kata ya Muhukuru, Kijiji cha Matama, Mkoani Ruvuma.
Vifaa hivyo, ni mifuko
800 ya saruji na nondo 400 zitakazosaidia kufanikiwa ujenzi wa kama njia
yakuleta maendeleo katika jamii.
Katika kufanikisha ujenzi
huo, NSSF imetoa mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo zipatazo 400.
Akizungumza katika hafla
ya makabidhiano hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji, alisema NSSF
ni shirika kubwa la hifadhi ya jamii lenye ofisi katika kila mkoa wa Tanzania
na wilaya zake.
Mpango wa ujenzi wa
zahanati hiyo umetokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa NSSF kuona jinsi
ya kusaidia jamii inayoshi katika Kata ya Muhukuru ambao walikuwa
wanatumia kilometa 62 kufika katika zahanati ya Muhukuru.
Msaada huo wa NSSF,
unalenga kufanikisha mpango huo wa kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za
afya, hivyo kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Mgeni rasmi katika hafla
hiyo ya kukabidhi vifaa vya ujenzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini,
Oraleti Komando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Naye Diwani wa Kata ya Muhukuru,
Manfred Mzuyu alisema msaada huo
umekuja kwa wakati muafaka kwani baada ya kukamilika, utapunguza kero
wanayopata wakazi wa kijiji cha Matama.
Aidha, diwani huyo aliongeza kuwa ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu
kuhakikisha hakuna atakayehujumu ujenzi wa kituo hicho na kutoa wito kwa
wengine kuiga mfano huo wa NSSF.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando,
akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 800 ya saruji na nondo 400 kutoka kwa
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, Mariam
Muhaji. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti
Komando, akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na NSSF kwa Diwani wa
Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma,
Mariam Muhaji.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam
Muhaji (wa tatu kulia), Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mmbaga
(wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengini wa NSSF
baada ya kukabidhi mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo 400 kwa ajili ya ujenzi
wa Zahanati katika Kijiji cha Matama, Songea.
Wakazi wa Kijiji cha Matama Kata ya Mahukuru
wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada wa mifuko ya saruji
iliyotolewa na NSSF kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matama,
Songea mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment