WADHAMINI
wakuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Benki ya NMB tarehe 28 ya mwezi April walifanya ziara katika makao makuu ya timu hiyo ‘Azam Complex’.
Ziara hiyo
ilikuwa na malengo makuu mawili, la kwanza ilikuwa ni kuwakutanisha mashabiki
wa timu hiyo na wachezaji nyota wa kikosi hicho, nahodha msaidizi Himid Mao
‘Ninja, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na beki kisiki Shomari Kapombe.
Wachezaji hao
walipata fursa ya kujibu maswali ya mashabiki kwenye zoezi ambalo lilikuwa
likiruka mubashara kwenye akaunti ya facebook ya ukurasa wa benki hiyo ‘NMB PLC
Tanzania’ na ule wa Azam FC.
Zoezi hilo la
kuwaunganisha mashabiki na wachezaji ni la kwanza kuwahi kufanywa na klabu
nchini, ambalo lilikuwa la kuvutia kutokana na vionjo mbalimbali na namna nyota
hao walivyokuwa wakijibu maswali.
Mara baada ya
kumalizika kwa mahojiano hayo, wafanyakazi wa benki hiyo kupitia timu yao ya
mpira wa mguu ilipata fursa ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana
wenye umri wa miaka 20 ‘U-20’ ya Azam FC, iliyoisha kwa NMB kukubali kwa taabu
kichapo cha mabao 7-3, huku ikishuhudiwa wakikosa penalti mbili.
Mchezo huo
ulikuwa mkali na wa aina yake sambamba na kuburudisha kutokana na ufundi
uliokuwa ukionyeshwa na timu zote uwanjani na watu waliokuwa wakishuhudia kila
mara walikuwa wakiinuka vitini na kushangilia.
Benki ya NMB
inayoongoza kwa sasa nchini ikiwa na matawi mengi yaliyosambaa nchini kote,
imekuwa na ushirikiano mkubwa wa udhamini na Azam FC kwa msimu wa tatu
mfululizo tokea msimu wa 2014/2015.
No comments:
Post a Comment