Kerengende wa
kike hujifanya wamekufa ili kukwepa tendo la ngono na wenzao wa kiume
Rassim
Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba aliona
kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya mapenzi,
akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale kerengende wa kiume
alipoondoka.
Ripoti hiyo
imechapishwa kwenye jarida la ikolojia.
Bwana Khelifa
amsema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa hawana ulinzi baada
ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende wengine.
No comments:
Post a Comment