KIPIGO
cha bao 1-0 kutoka kwa Simba jana katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) kinaifuta Azam FC
katika michuano ya Afrika mwakani.
Kwa
mara ya kwanza baada ya miaka mitano Azam FC itakosekana kwenye michuano ya
Afrika, ikitoka kushiriki Ligi ya Mabingwa mara moja na Kombe la Shirikisho
mara nne.
Unaizungumzia
timu yenye bajeti kubwa zaidi ya uendeshwaji kutokana na kuajiri wachezaji na
makocha wa gharama kubwa, wanaolipwa vizuri.
Timu
yenye viongozi wote wanaolipwa mishahara kwa sababu ni waajiriwa wa kampuni ya
Said Salim Bakhresa, wamiliki wa Azam FC na si wa kuchaguliwa na wanachama
wanaofanya kazi kwa ridhaa na utashi.
Timu
pekee yenye Uwanja wake rasmi ulioidhinishwa hadi na Shirikisho la Soka Afrika
(CAF) kwa mechi za kimataifa.
Azam
FC ndiyo klabu mfano wa kuigwa nchini na hiyo ndiyo klabu kubwa zaidi kwa
thamani na hadhi nchini, ukiachilia mbali ukubwa wa majina na umaarufu wa Simba
na Yanga.
Azam
hakikosekani kitu. Wachezaji siyo tu wanalipwa vizuri, bali wanalipwa kwa
wakati yaani wamiliki wanaihudumia timu vizuri, hakuna shaka.
Upande
wa pili, wachezaji wa Simba na Yanga wanatamani huduma ambazo wanazipata
wachezaji wa Azam FC. Mara kadhaa wachezaji Yanga wamegoma msimu huu
kushinikiza walipwe malimbikizo ya mishahara yao ya miezi kadhaa.
Azam
wamekwishatupwa nje ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na Jumamosi iliyopita
wametolewa kwenye Kombe la ASFC katika msimu ambao wamiliki walitoa fedha
nyingi mno kusajili wachezaji wapya na makocha wapya.
Mwanzoni
mwa msimu Azam ilileta jopo la makocha kutoka Hispania chini ya Zeben Hernandez
Rodriguez, ambao walifukuzwa baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu na kuletwa
Mromania Aristica Cioaba.
Waspaniola
walianza vizuri kwa kuipa timu ya Ngao ya Jamii, lakini wakawa na mwendo wa
kusuasua kidogo kwenye Ligi Kuu hata ikawa sababu ya kufukuzwa kwao, lakini
bahati mbaya mbadala wao naye hajafanya vizuri.
Msimu
huu Azam imebadili wachezaji wote wa kigeni, wakiondoka Waivory Coast Kipre
Balou, Kipre Tchetche, Serge Wawa, Mrundi Didier Kavumbangu, Mkenya Alan Wanga
na Mnyarwanda Jean Baptiste Muguraneza.
Mwanzoni
mwa msimu walisajiliwa ni Ya Thomas Renaldo kutoka Ivory Coast,
Daniel Amoah kutoka Ghana, Francesco Zekumbawira, Bruce Kangwa wote kutoka ambao waliungana na Mugiraneza, Wawa na Balou kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
Daniel Amoah kutoka Ghana, Francesco Zekumbawira, Bruce Kangwa wote kutoka ambao waliungana na Mugiraneza, Wawa na Balou kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
Lakini
katika dirisha dogo Desemba wakaachwa wote na kubaki Daniel Amoah na Bruce
Kangwa waliounganishwa na Samuel Afful, Daniel Atta Agyei, Yahaya Mohammed,
Yakubu Mohammed wote kutoka Ghana na Stephan Kingue kutoka Cameroon.
Zote
hizo ni fedha ambazo Said Salim Bakhresa ilizitumia katika mradi ambao bado
haujaanza kujiendesha.
Kampuni
pia iliongeza nguvu upande wa Watendaji baada ya kuajiriwa Meneja Mkuu, Abdul
Mohammed na watendaji wengine wadogo wadogo.
Lakini
mwisho mwa msimu, timu inakosa nafasi ya kucheza michuano ya Afrika mwakani kwa
mara ya kwanza baada ya miaka mitano.
Si
haba, imetwaa mataji mawili, kwani mbali na kuifunga Yanga katika Ngao ya
Jamii, pia iliifunga Simba katika fainali ya Kombe la Mapinduzi, lakini mataji
hayo yanawapeleka wapi?
Bila
shaka, Azam FC ipo katika msimu mbaya zaidi ndani ya miaka mitano na hii
inamaanisha kuna haja ya viongozi wa Azam FC kujitathmini, walikosea wapi?
No comments:
Post a Comment