MWIGIZAJI chipukizi
kutoka tamthilia ya Siri za familia Sharifa Mansoor ‘Shiffer’ amesema kuwa
uigizaji ni kazi sawa na kazi nyingine lakini walioanza walitumia fursa yao
vibaya kwa kufanya mambo yasiyofaa kujikita katika masuala ya kashifa kitu
kilichopelekea jamii kudharau fani hiyo.
Shiffer mwigizaji wa tamthilia ya Siri za Familia
“Haikuwa rahisi nilipoomba familia yangu kujiunga na
Siri za familia kila mtu alisema kuwa naenda kupotea lakini nilijieleza na
kukubaliwa sasa wananielewa nafanya kazi, shida waliotangulia walituharibia,”alisema.
Shiffer mwigizaji wa tamthilia ya Siri za Familia
Shiffer anasema kuwa wasanii waliotangulia walijisahau na kushindwa kulinda
heshima ya fani na kujikuta wengi wakiangukia katika kashifa na wao kuona ni
sehemu ya kujipromoti kumbe jamii inabaki na taswira mbaya kwa wasanii kama ni
watu wasio na faida katika jamii.
Shiffer mwigizaji wa tamthilia ya Siri za Familia
Tamthilia ya Siri za familia kwa sasa ndio igizo linalotamba na kuwaibua
wasanii nyota wengi wenye uwezo kama alivyo Shiffer na kuleta upinzani kwa
wasanii wakongwe ambao kwa sasa wamebanwa baada ya soko la filamu kuyumba na
kutoa nafasi kwa sinema za nje kuchukua nafasi.
No comments:
Post a Comment