Tuesday, May 2, 2017

WAZIRI LUKUVI AZINDUA MPANGO KABAMBE MTWARA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi akikagua mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi
katika Halmashauri ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa
ukamilifu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi akikagua masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya
Mtwara na kuwataka Maafisa Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi
katika mpangilio mzuri ili kuepusha migogoro ya ardhi..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa
Mpango Kabambe Mkoani hapo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego
(wakwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza
kulia), Mwenyekiti wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa
katika uznduzi huo.
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi
wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi.
Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa
ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya kuwasili mkoani humo.
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa
Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . Katika shughuli hiyo
Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa
kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha kuwa
wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya kusini yote
vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda.
Katika ziara
hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya
ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili
kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.
Aidha, Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri
Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango
kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara na watanzania kwa
ujumla.
Katika
uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi. Imaculate Senje
ameeleza kuwa uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au koundoa
kabisa tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara, na kuchochoea fursa za
uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara kufuata mpango huo kwa
maendeleo ya taifa.
Pia Ndugu
Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza kuwa dira ya
mpango kabambe huo ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa mafanikio ambao hutoa
kazi na fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.
Afisa huyo
ameeleza mpango huo umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe na Ziwani
ukigusa huduma zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na shughuli za
kiuchumi yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
BALOZI SEIF AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MCT
Older Article
MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 2, 2017
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment