Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem kwa
wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa
vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana
jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja
wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com
bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel,
Hamza Zuheri.
Meneja wa
Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia) Application ya
Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure baada ya kujiunga na huduma
mpya ya vifurushi vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na
Kampuni ya Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja
Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akisalimiana na Meneja
wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus mara baada ya uzinduzi
rasmi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni
hiyo jana jijini Dar es salaam, ambapo wateja wa Zantel watapata huduma ya
kusikiliza muziki bure kupitia application ya Mdundo.com
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wanafunzi
wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi
vya bure kwa mitandao yote ya kijamii yenye lengo la kuwanufaisha hasa vijana.
Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia
katikati ni Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.
Mtaalamu wa
masuala ya Biashara Zantel, Rehene Cathbert Tarimu (kulia) akionyesha
Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure mara baada ya
kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii
iliyozinduliwa na Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Mtaalamu
wa huduma za simu Emmilina Albert Vokolawene pamoja na Mtaalamu wa masuala ya
Teknolojia Zantel Salim Awadh.
Kampuni ya simu
inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya
ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti
zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.
Akizindua rasmi huduma
hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema
wateja wa Zantel wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi
watapata nafasi ya kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya
kusikiliza muziki bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.
Aliongeza kwa kusema
“Tunajisikia fahari kubwa sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni
mwendelezo wa jitihada zetu za kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha
wateja wetu wanaendelea kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya
intaneti ya kasi zaidi ya 4G Tanzania nzima.
Akifafanua zaidi kuhusu
huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza
Zuberi alisema, “Kwa wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na
mwezi ambavyo ni ;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa
2.5G watapata nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa
wateja wenye simu au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa
wateja wetu wanaotumia simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia
simu au vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar
es Salaam na visiwani Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.
Aliongeza kuwa baada ya
kufanya utafiti wa kina kwenye soko la mitandao ya simu waligundua kuwa vijana
wengi wanapenda muziki ambapo mpaka sasa hakuna kampuni yoyote ya simu inayotoa
huduma hiyo bure, na hivyo kuwafanya Zantel kuileta huduma hiyo sokoni kwa kupitia
‘Mdundo Music Application’.
’Mdundo Music
Application’ ni moja ya programu kubwa kabisa za muziki barani Afrika
inayowawezesha watu kuweza kusikiliza aina zote za muziki kwa kutumia intaneti.
Programu hiyo ina zaidi ya nyimbo 200,000 kutoka kwa wanamuziki zaidi ya
40,000. Zantel inaamini ofa hii itawafaa zaidi vijana kwakuwa wengi wao
wamekuwa kwenye utamaduni wa kisasa unaopenda ziaidi muziki na hivyo huduma hii
ya bure itawavutia zaidi.
Aliongeza kuwa huduma hiyo mpya inapatikana karibu kwenye mifumo yote ya simu za mkononi kama vile Android, iOS kwa ajili ya iPhone, Blackberry na Nokia Symbian.
Martin Nielsen, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mdundo.com alisema, “Wateja wa Zantel wanaweza kupata orodha yote ya nyimbo kupitia Mdundo ikiwa ni pamoja na nyimbo mchanganyiko zilizoandaliwa na Ma DJ maarufu, muziki wa Afrika Magharibi na pia Mashariki. Tanzania ni soko letu ambalo linakuwa kwa kasi sana na tunatarajia kuwa mpango huu utasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uharamia kwenye soko la muziki nchini na kuwapa wateja sababu ya kufurahia muziki zaidi ya hapo awali”.
Huduma hii mpya kutoka Zantel imekuwa miongoni mwa huduma nyingine za kibunifu na kidijitali ambazo zimeanzishwa na Kampuni hiyo hivi karibuni. Huduma hizo ni pamoja na uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G LTE upande wa Bara na Visiwani, ‘Zantel Madrasa’ huduma inayowawezsha waumini wa dini ya Kiislamu kupata mafundisho, Quran, Habari za BAKWATA na mawaidha mbalimbali ya kiislamu kwa njia ya simu, ikiwemo pia kwa njia ya SMS na ‘ Zantel Madrasa App’.

Akizungumzia uwekezaji wa
Zantel, Janin alisema wamewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 10 katika
uboreshaji wa mtandao ambapo mpaka sasa zoezi la maboresho hayo katia maeneo ya
Stone Town Zanzibar na Mkoa wa Mjini Magharibi yameshakamilika. Zoezi hilo
linaloendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba linaarajiwa kufikia
kikomo mwisho wa mwezi huu.

No comments:
Post a Comment