Mwanamapinduzi wa mrengo wa kushoto
Masaaki Osaka, amekamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la kumuuwa afisa mmoja wa
polisi, wakati wa maandamano yaliyofanyika katika barabara za mji mkuu Tokyo,
miaka 45 iliyopita.
Anadaiwa alimchoma moto afisa huyo kwa
bomu la petroli la kujiundia maarufu kwa jina Molotov Cocktail petrol bomb.
Hakuna mshukiwa wa uhalifu amewahi
ambaye amehepa vyombo vya usalama kwa muda mrefu kiasi hicho, vyombo vya habari
nchini Japan vimeripoti.
Serikali ya Japan haina hukumu ya
kifo.
Kifungo kirefu cha miaka 15,
kilifutiliwa mbali mwaka 2010.
Ni wapi wanaotoroka kutoka magerezani
na vifungoni hukimbilia?
Bwana Osaka alikamatwa mwezi uliopita
ndani ya nyumba moja mjini Hiroshima inayomilikiwa na Chukaku-ha, au makao ya
vuguvugu la Revolutionary Communist League (JRCL).
Tangu alipokamatwa, maafisa wa polisi
wanasemekana walimtaka anyamaze kimya.
Awali mtoro huyo alituhumiwa kwa kosa
la kuzuia polisi kufanya kazi yao- kabla ya polisi kung`amua alikuwa nani.
Mnano Jumatano wiki hii, alihamishiwa
Tokyo kutoka Hiroshima, ili kuhojiwa zaidi, hayo ni kwa mjibu wa taarifa za
vyombo vya habari nchini Japan.
Polisi inasema kwamba, imemtambua
kupitia uchunguzi wa DNA uliofanywa, kwa sababu alama ya vidole havikupatikana
wakati alipotekeleza uhalifu.
Wanasema kuwa Bw. Osaka aliweza
kufaulu kukwepa mkono mrefu wa sheria kwa miaka mingi kiasi hicho, kwa sababu
ni mmojawepo wa wanachama wa ngazi za juu wa vuguvugu hilo la mrengo wa kushoto
la JRCL na alisaidiwa na washirika wake.
Vuguvugu la JRCL, lilianzishwa miaka
ya 1950s na miaka ya 1960s na 1970s lilifahamika kwa kupanga maandamano mabaya
yenye ghasia.
Bw. Osaka anatuhumiwa kwa kumuuwa
afisa mmoja wa polisi mwenye umri wa miaka 21wakati wa ghasia mbaya katika kata
ya Shibuya, Jijini Japan mnamo mwaka 1971.
Inasemekana alimgonga kwa fimbo ya
chuma kabla ya kumteketeza.
Vuguvugu la JRCL linapinga vitu vingi,
vikiwemo hatua ya Marekani kujaza wanajeshi wake Japan.
Matukio makubwa yaliyotokea nchini
Japan muda wote Masaaki Osaka alikuwa mbioni:
1972 - Waziri mkuu wa Japan azuru
China na uhusiano wa kidiplomasia ukarejeshwa.
1993 - Serikali ikatoa taarifa ya
kihistoria maarufu "Kono statement" ikiomba msamaha kwa niaba ya
wanajeshi wake wakati wa vita kuu kuwatumia wanawake kama wafungwa wa ngono.
1995 -
Tetemeko la ardhi lagonga katikati mwa Japan, huku maelfu wakiuwawa.
2011 Februari - China ikaipiku Japan kama taifa la pili
kwa uchumi mkubwa duniani.
2011 Machi - Tetemeko kubwa lakumba
ufukwe wa Japan na kusababisha kabobo la Tsunami, huku maeneo mengi
yakiathirika vikiwemo vinu vya kinyuklia vya Fukushima na kusababisha kuvuja
kwa miale.
2014 - Serikali ya Japan, yaidhinisha
mabadiliko makubwa katika idara yake ya jeshi, na kuanzisha fursa ya majeshi
yake kutumika katika ujumbe wa kupigana nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment