Jeshi la polisi limethibitisha kuungana na wadau wa soka mkoa wa Dar es
Salaam katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wachezaji, viongozi, waamuzi,
mashabiki na mali zao wakati wote wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.
Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi amesema, jeshi la
polisi litatumia mbinu ya ulinzi shirikishi pamoja na wadau wengine wa vyombo
vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa mashindano.
Kamisha
msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano.
“Tumejipanga lakini tutakuwa na ullinzi shirikishi ambao utahusisha wadau
wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na vikundi mbalimbali vya ulinzi navyo
vitakuwepo. Tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona vijana wao,
wapate burudani na mwisho wa siku tupate kitu tunachokitarajia.”
“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jambo lolote kwenye
maisha ya kila siku, ulinzi na usalama ni suala mtambu na linahitaji
ushirikishwaji wa pamoja, makuindi yote katika jamii yetu tunatakiwa tushiriki
katika nafasi yake linahitaji kushiriki moja kwa moja katika ulinzi na
usalama.”
“Hata kwenye jeshi la polisi tunafanya michezo, tuna program moja
inaitwa michezo na vijana ambapo tumekuwa tunahamasisha vijana kuachana na
matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina mbalimbali.
Mratibu wa
michuano ya Ndondo Cup Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano,
kulia ni Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi.
“Kama mnavyofahamu, michezo inajenga ushirikiano, upendo na mambo mengi
lakini kubwa ni ajira. Vijana wengi hawana ajira kwa hiyo kwenye mashindano
haya tunategemea vipaji mbalimbali vitaibuliwa na kuwasaidia hapo badae kwenye
maisha yao.”
“Sisi kama jeshi la polisi tutakuwepo na tumekuwa na mahusiano na raia
enzi na enzi tangu kuanzishwa kwa jeshi la poilisi, hauwezi kututenga na raia
wala huwezi kuwatenga raia na askari. Kwa hiyo ushirikiano ni lazima uwepo na
uendelee kwenye masuala ya ulinzi na usalama.”
Michuano ya Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi inataraji kuanza rasmi
Jumamosi Juni 17, 2017 ambapo mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi
itazikutanisha Stimtosha dhidi ya Makuburi kwenye uwanja wa Kinesi.
No comments:
Post a Comment