Mkurungenzi wa Mkuu wa Tanzania Media Foundation
(TMF), Bw. Ernest Sungura aliyekaa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja
na washiriki wa kuchora vibonzo vijana muda mfupi baada ya kuzindua rasmi
warsha ya kuwajengea uwezo vijana katika Uchoraji wa Vibonzo, yanayoendelea
katika kiota cha wasanii cha NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam. Mafunzo
hayo yanatolewa na asasi ya Nathan Mpangala Foundation (NMF) na kufadhiliwa na
Ubalozi wa Uswis nchini. Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa NMF, B.
Nathan Mpangala wakati kulia kwake ni afisa utawala wa Nafasi Art Space.
Mafunzo yatamalizika kesho ambapo Balozi wa Uswis nchini tanzania, bi. Florence
Tinguely Mattli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Mwezeshaji Nathan Mpangala, akimwelekeza jambo
mmoja wa washiriki wa warsha ya karikacha na uchoraji vibonzo yanayoendelea
jijini Dar es Salaam.
Penye vibonzo hapakosi tabasamu.
Baadhi ya washiriki wakifanya yao.
Mchoraji, Said Michael maarufu kama ‘Wakudata’
akifanya yake.
No comments:
Post a Comment