Rapa Lil Wayne amefunguliwa mashtaka
yanayohusiana na ubaguzi wa rangi baada ya mlalamikaji kusema amepigwa ngumi ya
uso na rapa huyu na kutamkiwa maneno ya kibaguzi.
Mlalamikaji ni Mlinzi wa Club ya Hyde
mjini California anasema mnamo June 2016 Lil Wayne na kundi lake
walikuwepo kwenye club hio kwaajili ya After Party ya BET Music Awards na
ndio tukio hilo lilipotokea.
Mlinzi huyu anasema “Lil Wayne
alinirushia glasi ya pombe usoni na kusema maneno ya kibaguzi ambayo ni “F***
you white boy!” Maneno WHITE BOY yamepelekea kesi hii kuhusishwa na
Ubaguzi wa Rangi.
Camp ya Lil Wayne imekanusha taarifa
hizi huku askari huyu akidai fidia ya dola $25,000 za Kimarekani.
No comments:
Post a Comment