Dar es Salaam, Wateja wa Vodacom Tanzania PLC ambao ni watumiaji
wa huduma ya kifedha ya M-Pesa wameanza kunufaika na gawio la shilingi bilioni
7.9.Gawio hilo limeanza kuwanufaisha jumla ya watumiaji milioni saba wa huduma
ya M-Pesa nchi nzima.
Utoaji wa gawio unaendana na matakwa ya Benki kuu ya Tanzania. Hadi sasa
Vodacom tayari imeshatoa jumla ya shilingi bilioni 80 kama gawio ambalo
huhifadhiwa kwenye akaunti maalum ya M-Pesa Trust iliyopo kwenye benki za
biashara hapa nchini.
Kabla ya gawio la sasa, jumla ya Tsh bilioni 72 zilishagawiwa
katika awamu tofauti tangu kampuni hii ianze utaratibu wa kutoa gawio Mwezi
Disemba 2016. Utoaji wa gawio hufanyika kila baada ya miezi mitatu na gawio la
sasa ni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa biashara ya mtandao wa kampuni
hiyo,Sitoyo Lopokoiyit alisema “M-Pesa inamwezesha kila mteja kupata
huduma ya kifedha. Tunapojitahidi kumfikia kila Mtanzania, tunaendelea kutoa
huduma bora na za kisasa zinazoziwezesha Serikali na biashara kufanya kazi
pamoja na huku tukitoa faida nono kwa mawakala na wabia wetu,” alisema.
Mkurugenzi huyo aliwaasa wateja ambao tayari wameanza kunufaika na
gawio hili kutumia fedha hizo kununua Ukarimu bando ili waweze kunufaika
zaidi kimawasiliano kwa wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na
kufanya malipo ya moja kwa moja kutoka kwenye simu zao wanaponunua bidhaa na
huduma mbali mbali na kusititiza kwamba kwa sasa kuna mamia ya wakala
wanaopokea malipo kwa njia ya M-Pesa na APP mpya ya M-Pesa imefanya malipo kuwa
rahisi zaidi.
Lopokoiyit alifafanua kuwa, kiasi ambacho mteja anapokea kama gawio
hutegemeana na matumizi yake kupitia huduma ya M-Pesa kama kutuma pesa, kununua
muda wa maongezi, kulipa huduma na bidhaa pamoja na nyingine. Alisema Vodacom
itaendelea na jitihada za kuboresha maisha ya wateja wake kupitia huduma mbali
mbali mbali na kuwataka wateja wa Vodacom kuendelea kutumia huduma ya M-Pesa
ili waweze kunufaika na mambo mbali mbali ikiwamo gawio.
No comments:
Post a Comment