Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye
awamu ya pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya
VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel, Dar es Salaam jana.Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel,
Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi
tano mpya kwenye awamu ya pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi
kupitia programu ya VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akionyesha jinsi ya kutumia simu ya
mkononi kupata progaramu ya masomo ya mafunzo ya ufundi Stadi VSOMO wakati wa
uzinduzi wa programu ya pili ya mfunzo hayo jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano na Mkurugenzi wa VETA Kanda
ya Dar es Salaam, Habib Burko.
Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel kupitia application ya VSOMO leo wametangaza na
kuzindua kozi mpya za ufundi stadi za VETA zitakazotolewa kupitia simu za
mkononi ili kuwawezesha watanzania kujiunga na kupata utaalamu na vyeti vya
VETA kwa gharama nafuu
Kozi hizo mpya zinazoongezwa katika mfumo wa vsomo ni Huduma ya chakula
na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani,
ufundi Bomba wa Majumbani na Umeme wa magari.
Tangu kuzinduliawa kwa mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia
application ya VSOMO mwezi wa Juni 2016 ulianza kutoa kozi mbalimbali za ufundi
za VETA ikiwemo Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za
mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma
Ufundi wa kuchomea vyuma.
Lengo la mfumo huu likiwa ni kutimiza dhamira ya VETA ya kutanua wigo
wa mafunzo ya ufundi stadi nchini na kuongeza idadi ya vijana kujipatia fani mbalimbali
za ufundi ili waweze kuajirika au kujiajiri. Mafunzo haya yanawawezesha
wanafunzi kujisomea wakati wowote kwa gharama nafuu kupitia simu zao za mkononi
za Airtel.
Mfumo huu wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO, sasa ni maarufu
kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua
application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wanasoma kozi
mbalimbali zilizopo pia wapo waliomaliza na kupata vyeti vya VETA.
Akiongea wakati wa kuzindua na kutangaza kozi hizo, Mkuu wa chuo cha
Veta Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alisema “mafunzo ya ufundi kwa njia ya
mtandao ya VSOMO yametuwezesha kuongeza wigo na kuwafikia watanzania wengi
nchini. Tunaamini bado tunayofursa ya kuongeza wigo zaidi na kuongeza
idadi ya vijana wenye ueledi ili kwenda sambamba na agenda ya serikali ya awamu
tao ya uchumi wa viwanda kwa kupata nguvu kazi yenye taaluma muhimu katika
kuendesha uchumu wa nchi”
“Tunaamini kozi hizi mpya zitatawavutia vijana wengi kujiandikisha,
kusoma na kupata ujuzi zaidi.” Alisisitiza Eng Luteganya
Eng, Luteganya alisema kuwa “Ili kupata mafunzo ya VSOMO kupitia
Airtel, ukiwa na Airtel pakua application katika google play store, na
kujisajiri na kisha chagua kozi inayokidhi mahitaji yao.
Ili kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA,
wale watakaomaliza masomo yao nadharia kupitia VSOMO watafanya mtihani ili
kufaulu na kujiunga na mafunzo ya vitendo katika vituo vya VETA vilivyopo nchi
nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo
katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo”.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice
Singano Mallya alisema “Tunajisikia furaha kuongeza kozi nyingi zaidi katika
mfumo huu wa masomo kwa njia ya mtandao wa VSOMO kwani itatuwezesha
kufikia idadi kubwa ya vijana wanaosoma kwa kupitia simu zao za mkononi. Lengo
letu ni kuhakikisha tunakuwa na kozi nyingi ili kwenda sambamba na matarajio na
mahitaji ya wanafunzi na watanzania kwa ujumla”.
Tunapenda kuwapongeza wote waliojiunga na kumaliza kozi zao na kuhimiza
wote ambao hawajapakua application ya VSOMO kufanya hivyo kwa kujiandikisha
katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO kwa
gharama nafuu ya shilingi 120,000 tu na kulipia kwa njia ya Airtel Money
kwa kupiga *150*60#.
Tunapenda kuwahimiza vijana kutumia fursa hii na kujiunga na kozi na
kujisomea wakati wowote na mahali popote. kozi hizi zinazochukua hadi mienzi
mitatu kumalizika lakini pia zinaweza kuisha mapema kulingana na muda
utakaotengwa na mwanafunzi kuweka bidii ili kumaliza mapema.
No comments:
Post a Comment