Kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini
(TFF), Kamati ya Uchaguzi ya TFF, imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo
utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Zifuatazo ni sifa za wagombea:
1. Awe
raia wa Tanzania.
2. Awe na
kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).
3. Awe na
uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa angalau miaka mitano.
4. Asiwe
na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na
mbadala wa faini.
5. Awe na
umri angalau miaka 25.
6. Awe
amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika
uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la
kwanza.
7. Awe
muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji
wa majukumu na malengo ya TFF.
8. Anayegombea
nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada
moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi
(10:00) jioni.
No comments:
Post a Comment