Hit Maker wa “Beautiful Girls” Sean Kingston
ametangaza kufilisika na kwamba kwa sasa anaishi na mama yake.
Sean Kingston ametoa kauli hii baada ya kushindwa
kulipa pesa anazodaiwa na wakili wake ambazo ni dola za kimarekani 12500,
Tanzania ni zaidi ya milioni 24.
Sean anasema kwenye akaunti yake ya
benki ana dola $500 tu ambazo ni kama milioni 1 ya Tanzania.
Mwaka 2015, wakili James J. Gangitano alifungua
mashtaka dhidi ya Kingston, kwa kushindwa kumlipa pesa zake na Sean aliahidi
kumlipa January mwaka huu.
Baada ya kufunguliwa kesi ya madai na
wakili wake, Sean Kingston ameamua kujaza form ya kufilisika akionyesha kwa
sasa hana umiliki wa mali yoyote, anaishi na mama yake Janice Turner mjini Los
Angeles.
No comments:
Post a Comment