Unamkumbuka Bradley Lowery yule dogo
shabiki mkubwa wa Stoke City anayesumbuliwa na kansa? sasa taarifa kutoka kwa
mama yake mzazi zinasema bado wiki chache tu tumpoteze Bradley kutokana na
ugonjwa huo ambao madaktari wameshindwa kuutibu.
Kila mpenda soka habari hizi zinamtia
simanzi lakini mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Jermain Defoe hakika
anapitia wakati mgumu sana kutokana na habri hizi na amekiri kupatwa na simanzi
kubwa.
Inafahamika kwamba Defoe na Bradley
walikuwa na uhusiano mkubwa sana ndani na nje ya uwanja na baada ya mama mzazi
wa Bradley kutoa taarifa hizo imemfanya Defoe kuipigia simu familia ya Bradley
kila aamkapo.
“Kila asubuhi inapofika nalazimika
kumpigia simu mama yake na huwa ananiambia wako poa, ila nakosa hata maneno ya
kuongea kutokana na habari za Bradley kubakisha siku chache za kuishi dunia”
alisema Defoe.
Defoe ambaye atahamia katika klabu ya
Bournamouth hivi karibuni tayari ameshaanza kukumbuka nyakati za furaha
alizopitia na Bradley na anatamani Bradley aendelee kuwepo katika mechi zake
zijazo jambo ambalo ni gumu.
Bradley amekuwa akijitokeza sana
katika michezo ya Sunderland ili kumpa support Jermain Defoe lakini pia mwezi
March mwaka huu alikuwepo katika dimba la Wembley wakati England walipocheza na
timu ya taifa ya Lithuania.
No comments:
Post a Comment