Waandishi wawili wa habari wamesafiri
kutoka Ubelgiji kuja nchini kwa ajaili ya kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa
Mbwana Samatta anaecheza kwenye klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji.
Gauyentie Bogouet pamoja na Marc
Cornelissen ambao wanaandikia gazeti la Het Belang van Limburg na website ya
www.HBVL.BE wana siku tatu tangu wafika Tanzania na leo watatembelea familia ya
Mbwana Samatta.
Lengo kuu la safari yao ni kutaka
kujua kwa undani alipotoka Samatta njia alizopita kabla ya kutua Genk maisha na
tamaduni za taifa anakotokea.
“Tupo hapa kwa siku mbili sasa (jana)
tumekuja kwa ajili ya kutaka kujua zaidi kuhusu Samatta alipotoka alikopita na
namna alivyofanikiwa kufika Genk. Kesho (leo) tutatembelea nyumbani kwao kwa
ajili ya kukutana na familia yake,” alisema Cornelissen mara baada ya
kumalizika kwa mechi ya Tanzania vs Lesotho.
Waandishi hao walikuwepo kwenye mechi
kati ya Stars dhidi ya Lesotho na walishuhudia Mbwana Samatta akifunga goli
katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Huenda ziara yao ikawa na faida kwa
wachezaji wa Tanzania kwa sababu wamepata fursa ya kushuhudia mechi na kuwaona
baadhi ya wachezaji wakiwa katika kiwango bora katika mchezo huo hivyo huenda
katika ripoti yao wakashauri vilabu vya Ubelgiji kuja Tanzania kusaka vipaji.
No comments:
Post a Comment