Kama
wewe ni mtembeleaji mzuri wa kurasa za mitandao ya kijamii ya wasanii wa lebo
ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz, bila shaka umekutana na uhaba mzito
wa picha zinazowaonesha wakiwa klabu za usiku. Hii imetokana na marufuku
inayowakabili!
Mpishi
rasmi wa muziki wa WCB ndani ya Wasafi Records, mtarishaji Laizer amesema kuwa
moja kati ya sera za lebo hiyo, zinakataza wasanii pamoja na mtayarishaji huyo
kwenda kwenye klabu za usiku kula bata.
“Moja
kati ya vitu ambavyo tunakatazwa ni kwenda klabu za usiku, hii hairuhusiwi
kabisa,” Laizer aliiambia Twenzetu ya Times Fm. “Nadhani ni kwa sababu ya
brand, haitakuwa kitu kizuri kuona brand inazurula tu usiku kwenye klabu na
kama unavyojua klabu za usiku zina mambo mengi,” aliongeza.
Hata
hivyo alisema kuwa wasanii hao wanaruhusiwa kuingia klabu kama kuna kazi au
kuna mwaliko maalum utakaowasilishwa kwenye menejimenti kama mwaliko rasmi.
Endelea
kubang tu na ngoma za WCB kwenye klabu ya usiku unayoikubali zaidi, lakini
usitegemee kumuona Harmonize, Rich Mavoko, Raymond, Lava Lava hata bosi
mwenyewe Chibu Dangote wakila bata karibu na wewe ndani ya klabu hizo bila
mualiko maalum.
No comments:
Post a Comment