WATANI wa jadi Simba na Yanga watakutana Agosti 23
katika mchezo wa ngao ya hisani ikiashiria ufunguzi msimu mpya wa ligi kuu ya
Vodacom 2017/18.
Pazia rasmi la ligi hiyo litafunguliwa Agosti 26
ambapo mechi saba zitachezwa katika viwanja mbalimbali nchini ambapo
itamalizika Mei 20 mwakani kwa kupatikana bingwa mpya.
Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania (TFF) amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mchezo huo wenye kuvuta
hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi utafanyika kwenye uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
"Mchezo wa ngao ya hisani kati ya Simba na
Yanga utafanyika Agosti 23 kwenye uwanja wa Taifa ukiashiria kuanza kwa msimu
mpya wa ligi 2017/18 na wiki moja mbele itaanza rasmi," alisema Lucas.
Aidha Lucas amesema miamba hiyo itakutana tena
Oktoba 14 katika mchezo wa kwanza wa msimu kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa.
Ratiba ya michezo katika wiki ya kwanza ya ligi hiyo.
Agosti 26
Ndanda vs Azam FC
Mwadui FC vs Singida United
Mtibwa Sugar vs Stand United
Simba vs Ruvu Shooting
Kagera vs Mbao FC
Njombe Mji vs Prisons
Mbeya City vs Majimaji
Agosti 27
Yanga vs Lipuli
No comments:
Post a Comment