Thursday, July 13, 2017

WASHABIKI WA MUZIKI NCHINI WAZISUBIRI KOLABO MATATA ZA COKE STUDIO KWA SHAUKU
Msanii Rayvanny
(katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni.
Mwanamuziki Izzo
Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi, Kenya.
Baadhi
ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa
katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.
Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola
Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha
kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje,
washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu
mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia
luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba na kwa upande wa Tanzania
wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana
wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa
Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice
Kirya, Victoria Kimani na 2Face.
Katika msimu wa Coke Studio wasanii wanaoshiriki
wanatokea katika nchi za Kenya,Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda,
Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar,
Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon wakisindikizwa na mwanamuziki nguli wa
kimataifa kutoka nchini Marekani Jason Derulo.
Mbali na wasanii kutoka Tanzania wakali wengine wa
muziki kutoka nchi za Afrika wanaoshiriki msimu huu ni Khaligraph Jones na Band
Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda (
Uganda).
Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka
Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown
na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka
Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic,Bisa Kdei na
Worlasi kutoka Ghana
Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola ambayo
iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio ambalo umaarufu
wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina
yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi
mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya
30 barani Afrika na kuzidi kuifanya Afrika izungumze lugha moja tu ya muziki.
Imelielezea zaidi kuwa onyesho hilo kuwa lina lengo
la kukusanya pamoja wasanii na kuonyesha uwezo na vipaji vya muziki vilivyopo
Afrika ikiwemo kutoa fursa kwa wasanii chipukizi kufanya kazi na baadhi ya
wasanii na watayarishaji wa muziki wa kimataifa,vilevile Kuwakusanya wasanii
wanaofanya aina tofauti ya muziki, wanaotoka katika nchi tofauti za Kiafrika
kuwawezesha kutengeneza sauti ya Afrika kupitia burudani ya muziki.
Coca Cola Coke Studio pia inaleta burudani kubwa
kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana
kupitia muziki.
Tags
# BURUDANI
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
DIRISHA LA UFUNGUZI WA LIGI KUU VODACOM AGOSTI 23, NI YANGA VS SIMBA
Older Article
NBC WINS 2017-18 SUPERBRAND EAST AFRICA AWARD
RAIS MWINYI: ASANTENI WASANII WOTE KWA KUNIUNGA MKONO
Hassani MakeroJan 24, 2025Light Upon Light Summit in Zanzibar Set to Inspire and Unite Global Muslim Community12th & 13th October 2024.
kilole mzeeSept 30, 2024BENDI ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO TAMASHA LA USIKU WA WAFIA DANSI JIJINI DAR ES SALAAM
Hassani MakeroMay 12, 2022
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment