Meneja Uendeshaji wa kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa
vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa
ya Cartrack Tanzania, Bi. Jayne Nyimbo (katikati), akipanda miti pamoja na
baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Malaika
Village, katika hafla ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti ya
matunda na mboga mboga na kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula
ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo Mkuranga
mkoani Pwani mwisho mwa wiki.
WATANZANIA hususan wamiliki wa magari
wameshauriwa kufunga vifaa vya kidigitali kwenye magari yao vitakavyosaidia
upatikanaji wa magari yao kirahisi pindi yatakapoibiwa.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo katika hafla ya
kukabidhi misaada kwa kituo cha watoto yatima cha Malaika Children's
Village kilichopo Mkuranga, Pwani mwishoni mwa wiki.
Alisema wamiliki wa magari wanapaswa
kutumia vifaa vya kisasa ili pamoja na kusaidia upatikanaji wa magari yao
lakini pia wanaweza kujua mwenendo mzima wa magari yapo popote yaendapo.
"Dereva anakuaga anaenda
kariakoo njiani anabadilisha njia na kwenda uelekeo mwingine hivyo kukuongezea
gharama za matumizi ya mafuta, hivyo ukifunga kifaa cha Cartrack utaweza kujua
kila uelekeo wa gari lako lilipo," akasema.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa
matumizi ya vifaa vya Cartrack katika kusaidia upatikanaji wa magari
yaliyopotea umekuwa na mafanikio makubwa katika siku za karibuni ukizingatia
kuwa shughuli hizo wamekuwa wakiziendesha kwa ushikiriano wa karibu na jeshi la
polisi nchini.
"Wamiliki wa magari wasione
hasara kufunga vifaa vya usalama katika magari yao kwani mathalani kwa gharama
ya shs 60,000 kwa mwezi unaweza kuokoa hasara kubwa ambayo ingetokea pindi gari
lako litakapoibiwa au kwa matumizi mabaya ya madereva," aliongeza.
Akizungumza kuhusu msaada wao kwa
kituo cha Malaika Bi. Anna alisema lengo lao ni kujaribu kuwawezesha watoto hao
ili waweze kukabiliana na changamoto zao wenyewe.
"Tumekuja kuwasaidia kupanda
miti ya matunda kama miembe na michungwa, na kupanda mboga mboga kusudi waweze
kujiwezesha hata bila ya kusubiria misaada," alisema.
Naye Meneja wa kijiji hicho James
Kalinga alisema kituo chao chenye watoto 70 kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali kubwa ikiwa ni ukosefu wa fedha katika kuondesha shughuli mbalimbali
za kituo.
"Kuna watoto wanasoma shule ya
msingi mkuranga, kilomita sita kwenda na kurudi kwa miguu, tuna watoto wanasoma
shule za sekondari, uhaba wa nguo, viatu.. natoa wito kwa wadau wengine kuiga
mfano wa Cartrack ambao wametusaidia kutuonye njia ambayo watoto wanaweza
kujitegemea," alisema.
No comments:
Post a Comment