Msanii wa vichekesho Mzee Majuto amefunguka na
kusema sanaa imembadilisha maisha na kudai ameweza kujenga nyumba kubwa tatu,
ameweza kununua magari matano pamoja na kumiliki shamba lenye ukubwa wa ekari
tano.
Mzee Majuto amedai kuwa ameanza kufanikiwa katika
sanaa baada ua kuanza kujitegemea mwenyewe kwenye kazi zake, hivyo amedai kwa
mafanikio ambayo amepata sasa inatosha.
Ameamua kuachana na kazi hiyo ya kuingiza, ingawa
anasema matangazo yupo tayari kufanya ila si uigizaji tena.
"Zamani sanaa ilikuwa ya mkandamizano sana
lakini baadaye nilipata mafanikio nilikuwa sina nyumba saizi nina nyumba tatu,
nikaweza kuwa na magari matano hiace nne na Noah moja na nikaweza kusomesha
watoto wangu wengine wakifika mpaka chuo kikuu, nashukuru Mungu nimejenga
msikiti na madrasa nina shamba langu kubwa zuri tu, hivyo nasubiri safari
ambayo haina kipingamizi lazima tuondoke ambayo ni kufa, kwa hiyo saizi mimi
sanaa basi labda mtu akiniita kuna tangazo nitamfanyia tangazo lake nikimaliza
narudi shambani kwangu kumtumikia Mungu na kuomba toba" alisema Mzee
Majuto.
Wiki kadhaa zilizopita Mzee Majuto alifanyia
upasuaji kutokana na tatizo lake la ngiri lakini mpaka sasa anaendelea vyema.
No comments:
Post a Comment