Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Yanga, Charles Boniface Mkwasa amekiri kuwa klabu yao inadaiwa kodi na serikali
huku akiwataka mashabiki na wanachama wa jangwani kuwa watulivu katika kipindi
hiki.
Mkwasa amebainisha hayo leo baada ya taarifa
kuwepo taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu jengo lao kupigwa mnada siku ya
Jumamosi.
“Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa na ardhi
lakini tayari tulifanya nao mazungumzo na kukubaliana namna ya kulilipa kupitia
mapato yetu ya milangoni. Tatizo ni kwamba hapa katikati ligi ilisimama, lakini
hivi karibuni inaanza na tutaendelea kulipa, Tutatoa taarifa rasmi baadaye”,
alisema Mkwasa.
Mkwasa amesema kiasi wanachodaiwa ni kikubwa
lakini hakizidi shilingi milioni 500, huku akiweka wazi kuwa pesa wanayotakiwa
kulipa kwa mwaka ni shilingi milioni 59.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kupitia kwa kampuni ya udalali ya Msolopa Investmenst Limited leo imetangaza
kulipiga mnada jengo hilo endapo Yanga hawatalipa kabla ya Agosti 19, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment