Kampuni
ya simu ya Halotel kwa kushirikiana na Serikali imetiliana saini Mkataba wa
kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano
kwa wote (USCAF) tukio ambapo Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia
59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu hapa nchini.
UCASAF
kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko
huo ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano
katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu
yakifikiwa kwa haraka zaidi hivyo kwa hatua hiyo ya Halotel itawezesha huduma
hiyo kufika maeneo hayo.
Lakini pia
ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji
wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye
mawasiliano hafifu.
Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai, kabla ya kuanza kwa
hafla ya kutiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya
kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo
kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda
iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu. Pamoja naokatika picha ni Mkurugenzi wa
Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa (Katikati) akiwashuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai kwa
Pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter
Ulanga wakitia saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni
hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya
Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa
makampuni yote ya simu
No comments:
Post a Comment