Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki, Sabasaba Mashingi
akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki, Sabasaba Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamo hilo la Biashara.
AFISA Mtendaji Mkuu wa
TPB Benki Sabasaba Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia
huduma wanazozitoa hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua
wigo wa biashara zao.
Moshingi aliyasema hayo
leo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la biashara lililofanyika katika
Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe.
Kongamano hilo la
biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika mkoa
wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za
serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na wasomi.
“Niwaambie tu huduma
hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina mbalimbali
lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa mara
nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.
“Lakini pia
nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani Tanga
lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali tunazozitoa.
“Kwani Benki yetu ya TPB
imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua shughuli zake za
kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa ujumla “Alisema Moshingi.
Aidha pia alisema
wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ta tano kuipeleka
nchi kwenye uchumi wa viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa
vikiwemo vya mkoani Tanga.
Hata hivyo alisisitiza
umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la mafuta
uliozinduliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao
kama benki wapo tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo.
No comments:
Post a Comment