Jeshi la Polisi nchini kwakushirikiana na nchi ya
Korea Kusini lipo katika mpango wa kufunga kamera za usalama (CCTV Camera)
katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza vitendo vya uhalifu pamoja
na kupunguza idadi ya Askari wanaofanya doria.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa maadhimisho ya siku ya urafiki
kati ya Tanzania na Korea kusini ambayo imefanyika kwa kuwakutanisha baadhi ya
Askari Polisi waliowahi kupata mafunzo ya Upelelezi katika nchi hiyo.
Aidha IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi
litaendelea kutilia mkazo katika kuwapatia mafunzo wataalamu wake
wanaoshughulika na uhalifu kwa njia ya mtandao ili kuendana na kasi ya wahalifu
wa njia hiyo ambapo amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza
kuwabaini wahalifu wanaotumia mitandao kufanya uhalifu wao.
Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini
Tanzania Song Geum-Young amesema kufungwa kwa kamera hizo kutasaidia kwa kiasi
kikubwa kukabiliana na uhalifu ambapo amesema nchini Korea Kusini Kamera
zimesaidia sana kupambana na vitendo vya uhalifu.
Nchi ya Tanzania na Korea kusini zimekuwa na
ushirikiano katika Nyanja mbalimbali ambapo kwa Uapnde wa Jeshi la Polisi kila
mwaka Askari wawili wamekuwa wakienda kujifunza katika Jeshi la Polisi la Korea
Kusini.
No comments:
Post a Comment