Mchungaji Jackson
Sosthenes amechaguliwa kuwa askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es
Salaam kwa kura 110 kati ya 185 zilizopigwa na wajumbe wa sinodi wa kanisa
hilo.
Mchungaji Sosthenes
amemshinda Mchungani Patrick Bendera aliyepata kura 74, huku moja ikiharibika.
Uchaguzi huo umefanyika jana Jumamosi Desemba 23, 2017 katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Dar es
Salaam la Mtakatifu Albano lililopo Posta wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa dayosisi
hiyo, Yohana Sanga amesema uchaguzi umelenga kumpata askofu wa tano wa Dayosisi
ya Dar es Salaam anayechukua nafasi ya Dk Valentino Mokiwa.
Amesema walioshiriki
uchaguzi huo ni wajumbe wa Sinodi ambao ni mapadri, mashemasi, walei, wajumbe
wa vikao vya sinodi na wa idara katika dayosisi.
"Baada ya Dk Mokiwa
kuamriwa kujiuzulu nafasi hii ilishikiliwa na kasisi mkuu, Jerome Napera ambaye
leo amemkabidhi Canon Sosthenes,” amesema.
No comments:
Post a Comment