Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, December 22, 2017

Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa

live it love it
                                                           PRESS RELEASE
Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa
  • Wateja Wengine 28 Wajishindia Zawadi za TZS 500,000 Kila Mmoja.

Dar es Salaam, 22 Desemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa imewaibua jumla ya mamilionea saba (7) wapya  katika droo ya wiki hii ya promosheni yake inayoendelea ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’.

Washindi wengine 28 nao wamejinyakulia donge nono za kila siku za TZS 500,000 kila mmoja, na kufanya jumla ya wateja walipotakana hadi sasa kufikia 90.

Akitangaza washindi wa wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema kuwa pamoja na zawadi hizo za kila siku, wateja wa Tigo Pesa wana fursa kubwa ya kushinda zawadi kubwa za TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni ambapo washindi watajulikana usiku wa kuamkia mwaka mpya.
Kufikia sasa tumetoa until now we have given out Tzs 69 Million to 90 winners and we expect  to give out Tzs 51Million more to remaining 63 winners

‘Kufikia sasa tumtoa jumla ya TZS 69 milioni kwa washindi 90 na bado tuna zawadi za TZS 51 milioni zitakazotolewa kwa washindi wengine 63, ikiwa pamoja na mamilionea wapya tutakaowapata usiku  wa kuamkia mwaka mpya wa 2018. Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda, kwa hiyo nawaasa wateja wote wa Tigo wachangamkie fursa hii ya kutimiza ndoto zao za sikukuu na mwaka mpya’ alisema.

Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

Kuhusu Tigo:

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.

Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.   
  
Tigo ni kampuni ya pili kwa ukuwa nchini na imekuwa kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini

Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.  

Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.
………………………………………………………………………………………………………

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na: 
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano

Simu: +255 713 123431            Barua pepe: Woinde.shisael@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages