Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Moja limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC THEATRE Kama sehemu ya kuenzi jitiada za RC Makonda kuboresha Sekta ya Afya kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila kutumia pesa ya Serikali.
RC Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo mnamo March 13 siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa wakati mmoja na kuhudumia Wagonjwa 20 kwa siku.
RC Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo Wagonjwa walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa kikisababisha Maumivu Makali na Vifo vya Mama na Mtoto lakini kupitia jengo hilo vifo vinaenda kupungua.
Makonda ameishukuru GSM Foundation kwa kufanikisha Ujenzi wa Jengo hilo ambapo inakadiriwa Hospital ya Mwananyamala inapokea Wagonjwa kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na Kati ya hao ni Wajawazito wanaohitaji huduma ya Upasuaji.
No comments:
Post a Comment