Akizungumza leo na wafanya biashara hao pamoja na waandishi wa habari amesema amewaita kuwataarifu kuhusu uhamaji kutoka yadi za hapa mjini na kuhaia Kigamboni ambapo Serikali imetenga eneo hilo.
“Nimewaita leo kuwambia muda wa kuhamia Kigamboni umefika na huduma zote kule zitapatikana kuanzia barabara,maji umeme na kituo cha polisi kwahiyo nataka magari yote yahamie Kigamboni na nawapongeza sana ambao wameshahamia”amesema
Kwa upande wa wafanyabiashara hao walisema wanaomba waongezewe muda wa kuhamia Kigamboni ili waweze kujipanga zaidi ambapo Rc. Makonda amesema inabidi waende wote kwa pamoja.
Mmoja kati ya Wafanyabiashara hao aliyefahamika kwa jina la Chicago Matelephone alimuomba Rc. Makonda awape muda hadi kufikia mwezi wa tisa yeye na wengine wote watakua wamehamia katika maeneo hayo.
Baada ya ombi hilo Mkuu wa Mkoa akasema mwezi wa tisa ni mbali sana na maeneo hayo sio kwamba watalipia kwa mara moja ni baada ya miaka sita ndo wataweza kulipia na kuyamiliki kuwa yao lakini amekubari ombi hilo na ikifika mwezi wa tisa watu wote wawe wamehamia bila kipingamizi.
“Nimesikia ombi lenu sawa ila kuanzia tarehe moja mwezi wa kumi sitegemei kuona Show room za huko mitaani wote mnatakiwa kuwa maeneo ya Kigamboni ambapo pia mtafurahia. kufanya biashara huko kwani kila kitu kinapatikana huko” amesema
RC Makonda amesema ndani ya eneo hilo zitapatikana ofisi zote zinazohusiana na biashara za magari ikiwemo TRA, TPA, Bank, Garage, Sheli, Vituo vya polisi, Fire (ones stop center.)
Wafanyabiashara hao wamepatiwa ofa ya kufanya biashara Miaka mitatu kwenye eneo hilo pasipokulipa pamoja na fursa ya kuunganishwa na wauzaji wakubwa wa magari kutoka Dubai kwaajili ya kufanya ubia
No comments:
Post a Comment