KWA UNAYO YAFANYA RC MAKONDA MUNGU ANAKUONA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Thursday, February 1, 2018

demo-image

KWA UNAYO YAFANYA RC MAKONDA MUNGU ANAKUONA

IMG_5165
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo.

Ujenzi wa jengo hilo la kisasa ni jitiada za RC Makonda kuthamini na !kuwapa heshima Viongozi wa Dini kwa kuhakikisha wanafanyakazi katika mazingira mazuri na yenye hadhi kutokana na thamani na mchango wao mkubwa katika jamii. 

Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Nne pamoja na Ground floor lina Ofisi ya Mufti wa Tanzania, Ofisi ya katibu, VIP room, kumbi za mikutano, Ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri,Jiko,Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua pamoja sehemu ya Mapokezi. 

RC Makonda amesema kazi wanayofanya Viongozi wa Dini ni kubwa hivyo tunapaswa kuthamini kwa kuwaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi. 

Aidha RC Makonda amesema shauku yake ni kuona hadi mwezi wa Ramadhani jengo linakuwa limekamilika na kuanza kutumika. 

Aidha RC Makonda amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Amani Taifa na viongozi wake.

Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber amemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika Miaka 50 BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na lakisasa Kama hilo hivyo RC Makonda anaweka historia ya kwanza.

Mufti amesema jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya kuona hata haibu hata kupokea ugeni wa viongozi wa kislamu ulimwenguni.


Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja wamemuombea Dua RC Makonda pamoja na Rais Dr. John Magufuli kwa kuwezesha kujengwa kwa msikiti wa Mfalme wa Morocco wenye uwezo wa kuchukuwa watu 8,000 ampapo ujenzi unaendelea. 

MATUKIO KATIKA PICHA RC MAKONDA AKIKAGUA UJENZI HUO
IMG_5148
IMG_5191

IMG_5148

IMG_5149

IMG_5150

IMG_5151

IMG_5152

IMG_5155

IMG_5174

IMG_5193

IMG_5196

IMG_5207

IMG_5216

IMG_5232

IMG_5250

IMG_5252

IMG_5149
  Makonda akiwasili katika ofisi zinazojengwa

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *