WANANCHI WAMPONGEZA RC MAKONDA KWAKUONGEZA MUDA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, February 2, 2018

demo-image

WANANCHI WAMPONGEZA RC MAKONDA KWAKUONGEZA MUDA

IMG_4513Kutokana na idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameamua kuongeza siku moja hadi kesho ili kuhakikisha wananchi wote waliofika wanasikilizwa na kuhudumiwa.
1Akiongea kwa niaba ya RC Makonda, Mwenasheria wa ofisi ya mkoa wa Dar es salaam Fabiola Mwingira amesema idadi ya wananchi waliojitokeza ni kubwa* tofauti na matarajio lakini wamejitaida hadi sasa zaidi ya Wananchi 3,000 wamepatiwa huduma.

RC Makonda pia amewatangazia Wananchi wote waliosikilizwa na wanasheria kufika ukumbi wa Diamond Jubilee ifikapo Tarehe 10 February kuanzia Saa moja Asubuhi kwaajili ya kupatiwa mrejesho.

Taarifa za kuongezwa kwa muda zimepokelewa kwa shangwe na Wananchi ambapo wamemsifu RC Makonda kwa kutanguliza Utu mbele kwa kuhakikisha wanyonge wanaipata haki yao waliyotaabika kuitafuta kwa miaka mingi.

HONGERA RC MAKONDA KWA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS MAGUFULI.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *