Wednesday, January 31, 2018

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakiwa kujenga mazoea ya kunawa mikono.
Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa kunawa mikono (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na ni Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono, (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe, hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo wakiwa katika hafla hiyo
Wananchi wametakiwa kunawa mikono wakati wote kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko yatokanayo na maradhi kutokunawa mikono.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo katika hafla ya kufunga Mradi wa magonjwa wa kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono jijini Dar es Salaam Afisa Afya Wilaya kinondoni JOHN KIJUMBE amesema walianzisha Mradi wa Kunawa mikono Uliofadhiliwa na shirika la kimataifa kutoka Japan JICA,likishirikiana na kituo cha Afya Magomeni ukiwa na lengo la kutoa elimu ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza kwa Njia ya kunawa mikono .
Amesema Mardi huo ulianzishwa Julai na kuzinduliwa Septemba 25,2017 ambapo umekamili January 2018 ambapo ulilenga kutoa elimu ya kuanawa mikono mashuleni katika Wilaya ya Kinondoni ambapo waliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi pamoja na walimu na kubaini kuwa wananchi wanauelewa mdogo wa Kunawa mikono baada ya kutoka chooni,na kabla ya kula.
"Katika huu mradi tuliouanzisha chini ya shirika la kimataifa la Japan (JICA) likishirikiana na kituo cha Afya Magomeni tumeweza kutoa elimu kwa shule katika Wilaya ya Kinondoni na kubaini kuwa wanafunzi wengi hawana elimu ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kwa Afya zao na kusababisha magonjwa ya Milipuko "Amesema Kijumbe.
Aidha amebainisha changamoto walizokumbana nazo ambapo amesema watu wanachukulia kunawa mikono siyo jambo muhimu, pamoja na ukosefu wa vifaa vya kunawa mikono katika jamii na mashuleni pia, hivyo amesema mradi huo utakuwa ni endelevu kwa jamii ili kuweza kukuza elimu hiyo ya kunawa mikono.
Pia amesema katika mradi huo wamepata mafanikio mbalimbali ambapo wameweza kufunga vifaa vya kunawia mikono kwa baadhi ya shule.
Kwa upande wake mratibu wa Mradi huo Rose Temu amesema Mradi huo utakuwa emdelevu na kutoa wito kwa watanzania kujenga mazoea ya kunawa mikono unapotoka chooni na kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Tags
# KITAIFA
Share This
About kilole mzee
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
KWA UNAYO YAFANYA RC MAKONDA MUNGU ANAKUONA
Older Article
Zawadi kem kem promosheni ya Jero Yako ya Zantel
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment