Na Florah Raphael.
Chama cha wananchi CUF leo kimetoa maamuzi ya kikao cha kamati tendaji iliyokutana machi 25 mwaka huu katika ukumbi wa ofisi ya wabunge wa CUF uliopo magomeni, Dar es salaam chini ya uenyekiti wa katibu mkuu.
Akiongea na vyombo vya habari katibu wa chama hicho Seif Shairf Hamad amesema kuwa, katika kikao hicho yalitolewa maamuzi mbalimbali kutokana na ajenda zilizokuwepo mezani ambapo kuhusu ajenda ya uhujumu wa chama cha CUF kamati iliamua chama kiendelee kufuatilia hujuma hizo kwa lengo la kudhibiti pia iliagiza viongozi wa ngazi zote kuwa makini na kufuatilia hila zote za kukihujumu chama na kuwafichua wale wote wanaopanga njama hizo.
Aidha ameongeza kuwa katika ajenda hiyohiyo waliamua kuwahimiza wanachama kuimarisha umoja, ushirikiano na mshikamano huku wakitambua kuwa umoja ni silaha mujarabu ya kuwashinda maadui wa chama.
Pia amesema kuwa katika ajenda ya taarifa kuhusu maendeleo ya kesi za chama, kamati inawapongeza mawakili wanaokiwakilisha chama katika kesi hizo kwa kusimamia kwa dhati na kwa weledi wa hali ya juu na kuongeza kuwa kamati inawaomba wanachama hasa wanaoishi jiji la Dar es salaam na viunga vyake waendelee kujitokeza kwa wingi mahakamani kila siku ambayo kesi inasikilizwa.
Kuhusu hali ya usalama nchini Seif amesema kuwa kamati iliamua kuendelea kufuatilia kwa makini malalamiko ya wananchi yanayotolewa kuhusu ukiukwaji wa haki zao kisha kushauriana na wadau wote ikiwemo serikali ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo na kubaini chanzo chake ili kutokomeza kabisa hali hiyo, kuikumbusha serikali kuwa jukumu lake la msingi ni kulinda usalama wa raia na mali zao ili jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi vijiimarishe kutimiza wajibu huo kwa weledi.
Pia ameongeza na kusema kuwa kuhusu hali ya usalama nchini kamati pia iliamua kuwakumbusha wananchi watimize wajibu wao na kutetea hali na kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na amani kwa kutofumbia macho vitendo vyote viovu vinavyoweza kuitikisa misingi madhubuti ya taifa letu, ikiwemo umoja na mshikamano.
Mwisho kamati ya utendaji wa Taifa ilitoa wito kwa watanzania wote kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake na kuendelea na utamaduni wetu wa kuhurumiana na kushirikiana katika wakati wa majaribu na wakati wa furaha.
Aidha Kutokana na matokea hayo katibu wa CUF wilaya ya kinondoni mohamed s. Mikandu ametoa malalamiko juu ya katibu wa chama hicho Seif Shairf Hamad kufanya kongamano lililofanyika kata ya Tandare bila kumshirikisha na kusema kuwa kongamano hilo halikuwa la chama bali walitumia jina la chama ili kufanikisha malengo yao binafsi na kuongeza kuwa kongamano hilo halikufuata utaratibu wa chama.
No comments:
Post a Comment